Thursday, April 20, 2017

Jogoo, ABC, Pazi zatakata RBA -VIDEO

By Oliver Albert, Mwananchi

Dar es Salaam. Jogoo  imeifunga Mgulani kwa pointi 84-53, huku ABC ikichakaza TZ Prisons pointi 75-55 katika mchezo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu inayoendela kwenye Uwanja wa Ndani  wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo mwingine uliochezwa saa 2:00 usiku, Pazi iliichapa Chui kwa pointi 71 -48.

Hadi sasa mabingwa watetezi Savio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 22 wakifuatiwa na Vijana City Bulls wenye pointi 21 wakati Ukonga Kings  ya tatu ikiwa na pointi  19.

Sylvian Yunzu  wa Savio ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga pointi nyingi akiwa amefunga pointi 195 hadi sasa akifuatiwa na  Ally Hashim wa Ukonga Kings aliyefunga pointi 186 wakati Yassin Choma wa  Kurasini Heat  akiwa nafasi ya tatu kwa kufunga pointi 181.

Pia, Yunzu anaongoza kwa wachezaji mahiri wa kufunga kwa kutumia  mitupo mitatu (Three pointi) akiwa amefunga mara 43 akifuatiwa na Erick Lugora wa  Oilers aliyefunga mara 23 na Frank Majura wa ABC akifunga mara 22.

 

-->