Asubuhi tu Simba waujaza Jamhuri

Dodoma. Saa matano kabla ya kuanza mechi ya fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao,  mashabiki wa Simba wameshauteka Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mashabiki  hao ambao wametoka maeneo mbalimbali nchini, walianza kumiminika uwanjani hapo kuanzia saa moja asubuhi wakiwa na mavazi yenye rangi zinazotumiwa na timu hiyo.

Kivutio zaidi ni vikundi mbalimbali vya ngoma vinavyoundwa na mashabiki wa timu hiyo ambavyo vimekuwa  vikitumbuiza nje ya uwanja.