Conte: Kiwango cha Neymar bado

Muktasari:

  • Mmiliki wa Chelsea, Abramovich anasubili kocha wake Mtaliano amuonyesha ni mchezaji gani anataka kumsajili kwa lengo la kuhimalisha klabu hiyo mwisho wa msimu, lakini cha kushangaza amemkataa Mbrazili huyo.
  • Abramovich anawasiwasi kuwa Inter Milan inaweza kumnyakuwa Conte kutoka Stamford Bridge, ambako watampa maisha mazuri na uhuru wa kuchagua wachezaji awapendao.

London, England .Antonio Conte ametupilia mbali uwezekano wa kumsajili Neymar, pamoja na bilione Roman Abramovich kuwa yupo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya kumsajili nyota huyo wa Barcelona.

Mmiliki wa Chelsea, Abramovich anasubili kocha wake Mtaliano amuonyesha ni mchezaji gani anataka kumsajili kwa lengo la kuhimalisha klabu hiyo mwisho wa msimu, lakini cha kushangaza amemkataa Mbrazili huyo.

Abramovich anawasiwasi kuwa Inter Milan inaweza kumnyakuwa Conte kutoka Stamford Bridge, ambako watampa maisha mazuri na uhuru wa kuchagua wachezaji awapendao.

Kwa mujibu wa gazeti la mji waTurin 'Tuttosport', mmiliki wa Blues amefikia makubaliano ya mdomo miamba ya La Liga kuhusu kumsajili nyota huyo mwenye miaka 25, kwa gharama inayokadiwa kufikia pauni155.5milioni.

Lakini kocha huyo wa zamani wa Juventus na Italia angependa kwanza kutegeneza kikosi chake cha sasa kabla ya kusajili mchezaji yeyote mpya na bado haamini kuwa Neymar atafaa katika mtindo wake wa uchezaji.

Neymar ameshindwa kuonyesha uwezo wa kufunga mabao msimu huu katika kikosi cha Luis Enrqiue, mwaka jana alifunga mabao 31, katika mashindano yote pia mwaka juzi alifunga mabao 39, lakini msimu huu amefanikiwa kufunga mabao 14 hadi sasa.

Sasa Chelsea ina nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujiao, inaamini wataweza kumsajili mchezaji yeyote wamtakae.

Chelsea kwa sasa inashikiria usukani wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 69, kumi zaidi ya Tottenham Hotspur inayoshika nafasi ya pili.