Kocha Mcameroon wa Simba aanza tambo

Kocha wa Simba, Joseph Omog

Muktasari:

Akizungumza katika mahojiano mafupi baada ya mechi ya kirafiki kati ya Simba na Moro Kids, Omog alisema kuwa kwa takribani wiki tatu za maandalizi yao mkoani Morogoro wachezaji wameiva na wana uwezo wa kufanya lolote wakati wowote.

Morogoro. Kocha wa Simba, Mcamroon, Joseph Omog amesema kikosi chake kiko tayari kupambana na  timu yoyote.

Akizungumza katika mahojiano mafupi baada ya mechi ya kirafiki kati ya Simba na Moro Kids, Omog alisema kuwa kwa takribani wiki tatu za maandalizi yao mkoani Morogoro wachezaji wameiva na wana uwezo wa kufanya lolote wakati wowote.

“Tulikuwa na mazoezi makali, kwa wiki mbili tulikuwa na mazoezi ya fiziki na wiki ya tatu ikawa ni ufundi na tumecheza mechi mbili za kirafiki …mchezo wa kwanza tuliifunga Polisi Morogoro mabao 6-0 na wa pili Moro Kids 2-0 tumeangalia vyote na sasa tunaamini wachezaji wako vizuri,” alisema.