Simba yamshukuru Mo

kwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) .

Muktasari:

  •  Mo aliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa klabu hiyo wakati huu Simba ikiandaa muundo wa marekebisho ya uendeshaji ambao utampa fursa ya kuwekeza ndani ya klabu hiyo.

Dar es Salaam. Klabu ya Simba imetoa pongezi kwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) kwa kuanza kutekeleza ahadi ya kulipa mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi na sekretarieti sambamba na kulipia kodi nyasi bandia kwa ajili ya ujenzi ya uwanja wa klabu hiyo.

 Mo aliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa klabu hiyo wakati huu Simba ikiandaa muundo wa marekebisho ya uendeshaji ambao utampa fursa ya kuwekeza ndani ya klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari na Mwasiliano wa Simba, Haji Manara ilisema uongozi unatambua juhudi zinazofanywa na Mo kuisadia klabu.

“Tunamshukuru Mo hasa ukizingatia kipindi hiki ambacho klabu haina mdhamini. Klabu inaamini uwekezaji huu ni chacu ya kuwarejeshea furaha wanasimba ya kutwaa ubingwa msimu huu ni misimu mingine inayokuja,”