Stand na ndoto ya ushindi

Muktasari:

Stand inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, imeruhusu mabao tisa katika mechi 12 ambazo imecheza hadi sasa.

Dar es Salaam. Klabu ya soka ya Stand United ya Shinyanga ina ndoto za kumaliza ligi ikiwa kwenye nafasi tatu za juu na kuihofia safu yake ya ulinzi kuwatibulia mipango hiyo.

Stand inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, imeruhusu mabao tisa katika mechi 12 ambazo imecheza hadi sasa.

Kocha wao, Athuman Bilali au ‘Bilo’ amesema safu yake ya ulinzi imekuwa ikifanya makosa ambayo kama yasiporekebishika, huenda yakaigharimu timu.

“Nina kazi kubwa ya kuirekebisha safu ya ulinzi kwa sababu imekuwa ikifanya makosa ambayo yamekuwa yakitoa nafasi kwa timu pinzani kufunga mabao kama ilivyotokea kwenye mechi zetu mbili za hivi karibuni.

Sina tatizo na nafasi nyingine za kiungo na ushambuliaji kwani zimekuwa zikitimiza majukumu yao kwa ufasaha,” amesema.