Uwanja wa Ndege kuitwa Maradona

Cristiano Ronaldo.

Muktasari:

Heshima hiyo inatokana na mafanikio makubwa ya ‘mtoto wao’ Ronaldo kwa mji huo na taifa lake, Ureno baada ya kutwaa taji la Euro 2016.

Madeira, Ureno. Uongozi wa mji wa Madeira Ureno umekubaliana kubadili jina la   uwanja wao wa ndege na kuuita Cristiano Ronaldo, kwa heshima ya nyota wao.

Heshima hiyo inatokana na mafanikio makubwa ya ‘mtoto wao’ Ronaldo kwa mji huo na taifa lake, Ureno baada ya kutwaa taji la Euro 2016.

Rais wa mji huo, Miguel Albuquerque alithibitisha uwanja huo utaitwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cristiano Ronaldo. Kwa  sasa, Ronaldo anamiliki hoteli nne tofauti mjini Madeira.