Watoto wa Julio kutoka Qatar wamuunga mkono uamuzi wa kugombea TFF

Muktasari:

  • Watoto hao wanaokipiga katika klabu ya Al Gharafa ya nchini Qatar wapo nchini kwa ajili ya mapumziko na ndipo wamekutana na suala zima la uchaguzi wa TFF huku baba yao akiwa miongoni mwa wagombea.

Watoto wa kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio', Hossam na Super wamempa baraka zote baba yao ambaye amejitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuchukua fomu ya ujumbe wa kamati ya utendaji.

Watoto hao wanaokipiga katika klabu ya Al Gharafa ya nchini Qatar wapo nchini kwa ajili ya mapumziko na ndipo wamekutana na suala zima la uchaguzi wa TFF huku baba yao akiwa miongoni mwa wagombea.

Waliliambia gazeti hili kuwa, kuchukua fomu kwa baba yao hakujawashtusha kutokana na jinsi ambavyo yupo karibu na masuala ya soka.

Hivyo inawezekana kabisa kuna upungufu ameuona kwenye soka la Tanzania.