VIDEO: Mizigo ya waliokufa, manusura wa ajali ya MV Nyerere yaanza kuelea

Mizigo zaidi inasukumwa ufukweni kutoka ndani ya kivuko cha Mv Nyerere baada ya wataalam kufanikiwa kukinyanyua na kukilaza ubavu

Muktasari:

Mizigo iliyokuwa ndani ya kivuko cha Mv Nyerere vimeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya ambako shughuli za uokoaji zinaendelea


Ukara. Baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi  iliyokuwa ndani ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozana ziwa Victoroa imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Hali hiyo imejitokeza baada ya wataalam wa uokoaji kufanikiwa kikilaza ubavu kivuko hicho hicho kilichopinduka Septemba 20 na kujifunika kifudifudi.

Kazi ya kunyanyua kivuko hicho inafanywa na wataalam kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakishirikiana na maofisa kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza.

Soma zaidi:

Operesheni ya uokoaji tayari imefanikisha kuopoa miili ya watu 226 waliokufa katika ajali hiyo, huku wengine 41 wakiokolewa hai.