Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Mke, mume wakutana kwa Makonda

WANAUME NAO WAJISOGEZA KWA MAKONDA KUDAI HAKI

Muktasari:

Katika tukio la leo, Aprili 10, Mwanamke, Sylvia Felisiano, alitinga katika viwanja vya ofisi ya RC Makonda, baada ya kusikia mume wake amekwenda kulalamika kuwa amekimbia na watoto wao watatu.


Dar es Salaam. Mapya yameendelea kuibuka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya wazazi wawili kukutana ana kwa ana katika ofisi hizo.

Kuanzia jana asubuhi, wanawake waliotelekezwa na wenza wao walifurika katika ofisi ya RC Makonda kama alivyoagiza ili kuwasaidia kisheria.

Katika tukio la leo, Aprili 10, mwanamke, Sylvia Felisiano alitinga katika viwanja vya ofisi ya RC Makonda, baada ya kusikia mume wake amekwenda kulalamika kuwa amemkimbia na watoto wao watatu.

Awali, mwanaume, Tito Chembs, alifika kwa mkuu wa mkoa akilalamika kuwa mke wake amempokonya watoto na kwenda nao Bukoba.

Saa chache baadaye, Sylvia alipata taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na kutinga katika ofisi hizo.

Maofisa ustawi wa jamii waliokuwa wakisikiliza mashauri hayo, waliwachukua wenza hao na kuingia nao ndani, huku Sylvia akionekana mwenye hasira na kuahidi ataongea kwa kina na wanahabari.

MCL Digital itaendelea kukujuza kwa kina yanayojiri kutoka katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa.