Mkutano wa TNBC kutoa mwelekeo wa uchumi Tanzania

Muktasari:

Kuna mabadiliko ya  kisera yamefanyika chini ya Rais tangu  ashike uenyekiti wa TNBC

 Mkutano wa  Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC) utatoa majibu yatakayosaidia kuchochea na kuweka mazingira mazuri katika azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda.

Katibu Mtendaji wa TNBC, Mhandisi Raymond Mbilinyi amesema kuna mabadiliko
mengi yamefanyika tangu Rais John Magufuli aongoze kikao cha kwanza cha 10 mwaka jana.

“Kuna mabadiliko ya  kisera yamefanyika chini ya Rais tangu  ashike uenyekiti wa TNBC, mfano ni kuanza kufanyika shughuli za bandari kwa saa 24. Mizigo hailalamikiwi kwa sasa inatoka muda wote na wafanyabiashara wanaridhika na utendaji,” amesema  Mhandisi Mbilinyi.

Ameongeza kuwa kumekuwapo na mikutano ya kupanga mikakati ambayo kwa kiasi kikubwa imewaweka karibu wadau wa biashara wakiwamo maofisa wa juu wa Serikali na sekta binafsi ambapo muunganiko huo umesaidia kuwapo kuaminiana kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika ujenzi
wa mazingira bora ya kufanya  biashara.

“Mijadala inayofanywa na TNBC inaisaidia Tanzania kufikia dhamira ya kuwa na viwanda na uwekezaji mkubwa mambo yanayopigiwa kelele na mwenyekiti wa Baraza, Rais Magufuli. Hali hii itaongeza ajira mpya na kufungua fursa za biashara mpya,” amesema  Mbilinyi.


Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi la Dunia (ILO) zinaonyesha kuwa sekta zisizo rasmi  zinachangia asilimia 41 ya GDP katika mataifa yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Sekta hiyo inatajwa kuchangia asilimia 60 ya uchumi katika mataifa ya Tanzania na Nigeria.

Katika kuliona hilo, TNBC katika mkutano wa kikao chake cha 10, iliona changamoto hiyo na kwa dhati walipitisha azimio la kutumia kitambulisho cha Taifa pamoja na namba ya mlipa kodi kwa sekta zisizo
rasmi kupitia Nida na TRA ili shughuli yoyote ya kiuchumi inayofanyika Serikali ipate kodi yake