Msimamizi wa uchaguzi Bunda Mjini akiri makosa kortini

Muktasari:

Akihojiwa na wakili wa upande wa mjibu maombi wa pili, Tundu Lissu kwenye kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo inayoendelea mjini hapa jana, msimamizi huyo alidai siku ya kutangaza matokeo hakuwa amelala tangu tarehe 24 usiku hadi muda ambao alitangaza matokeo saa 11:11 jioni.

Musoma. Msimamizi mkuu wa uchaguzi kwenye Jimbo la Bunda Mjini mwaka 2015, Lucy Msoffe amekiri kufanya makosa ya kuandika idadi ya wapigakura wakati wa kutangaza mshindi wa nafasi ya ubunge.

Akihojiwa na wakili wa upande wa mjibu maombi wa pili, Tundu Lissu kwenye kesi namba moja ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo inayoendelea mjini hapa jana, msimamizi huyo alidai siku ya kutangaza matokeo hakuwa amelala tangu tarehe 24 usiku hadi muda ambao alitangaza matokeo saa 11:11 jioni.

Alisema kutokana na uchovu  ndiyo maana alikosea kuandika idadi ya wapigakura mara mbili mfululizo wakati wa kutangaza mshindi.

Soma habari zinazohusiana