Mteule mwingine wa Trump amgomea

Muktasari:

Mapema mwezi huu, mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa.


Dar es Salaam. Kiongozi mwingine aliyeteuliwa na Rais Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji, Philip Bilden amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi.

Mapema mwezi huu, mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Bilden ameeleza wasiwasi alionao kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake.

Jim Mattis ambaye ni  waziri wa usalama  amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden ndani ya siku chache zijazo.