Mwanafunzi apewa kipigo Moshi

Muktasari:

Imeelezwa kuwa mwanafunzi huyo hufanyiwa hivyo na bibi yake

Moshi. Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Sokoine, Wilaya ya Moshi ameshambuliwa na vijana wawili baada ya kumfungia kwenye mti na kumpa kipigo hali iliyomsababishia kupata majeraha mwilini.

Mtoto huyo anayeishi na bibi yake, mtaa wa KCMC Rau alipewa kipigo hicho leo Ijumaa baada ya bibi yake ayenaishi naye kudaiwa  kutoa maagizo kwa vijana hao kufanya hivyo.

Shuhuda wa tukio hilo, Emanuel Shirima amesema kuwa mtoto huyo alipigwa baada ya kwenda kuogelea.

Amesema kuwa mtoto huyo sio mara yake ya kwanza kupewa kipigo na huyo bibi yake huyo.

"Yaani huyu mtoto ana kama mwaka hivi anapigwa na kunyanyaswa na huyu bibi," amesema shuhuda huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema hana taarifa yoyote.

Hata hivyo, Kamanda Issa amesema atafuatilia suala hilo kwa kuwa limetokea leo Ijumaa jioni .