Mwenyekiti akiri kutafuna Sh1 milioni za kijiji

Muktasari:

  • Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kijijini hapo, wanakijiji walisema hawana imani naye kwa sababu amekuwa kikwazo kwenye shughuli za maendeleo.
  • Mkazi wa kijiji hicho, Daud Mwanjonde alisema  katika vikao vyao na mwenyekiti huyo, alikiri kutumia fedha za miradi ya maendeleo hivyo hawana sababu ya kuendelea kuwa na kiongozi ambaye ni mbadhirifu wa mali ya umma.

Mbeya. Mwenyekiti wa Kijiji cha Iwindi wilayani Mbeya, Abraham Kamwela amekiri kutumia Sh1 milioni za kijiji hicho kwa matumizi yake binafsi baada ya wananchi kumtaka aachie ngazi.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kijijini hapo, wanakijiji walisema hawana imani naye kwa sababu amekuwa kikwazo kwenye shughuli za maendeleo.

Mkazi wa kijiji hicho, Daud Mwanjonde alisema  katika vikao vyao na mwenyekiti huyo, alikiri kutumia fedha za miradi ya maendeleo hivyo hawana sababu ya kuendelea kuwa na kiongozi ambaye ni mbadhirifu wa mali ya umma.

Akizungumzia tuhuma hizo, mwenyekiti huyo alidai kuwa alikwisha waeleza wanakijiji kuwa atazirudisha fedha hizo kwa kukatwa kwenye mshahara na posho zake.