Nape: Nia yetu kuona tasinia ya habari inakua

Muktasari:

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya radio duniani Nnauye amesema nia ya serikali ni kuhakikisha tasnia ya habari inakua.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali ipo tayari kufanya marekebisho yoyote ya sheria ya habari inayoonekana kukwaza ukuaji wa tasnia ya habari.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya radio duniani Nnauye amesema nia ya serikali ni kuhakikisha tasnia ya habari inakua.

Nnauye amewataka waandishi wa habari nchini kuzisoma sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ili kuwa na uelewe mpana wa mambo mengi utakaowasaidia kuandika mambo kwa upana na wakiwa na ufahamu nayo.

"Zisomeni sheria,  taratibu na kanuni, tulizonazo na kunielewa...kama ipo inayoonekana kukwaza tasnia ya habari, wizara ipo tayari kukaa chini na kuifanyia marekebisho," amesema Nnauye.

Alisema kumekuwa na changamoto ya wanahabari kuchukua kitu kimoja na kukimbia nacho kukieneza huku wakiwa hawajui ukweli halisi kutokana na kutokuzisoma sheria.