Ndanda yaishusha Njombe Mji

Muktasari:

Simba ndiyo bingwa wa ligi kuu msimu huu ,  kwa Wekundu wa Msimbazi hao, huo ni ubingwa wa 19 tangu mashindano hayo yaanzishwe.


Ndanda FC imeutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani wa Nangwanda Sijaona baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 3-0 na sasa imebakisha pointi moja tu ibaki ligi kuu.

Timu hiyo ambayo sasa itashika nafasi ya tatu kutoka mkiani na pointi 26, wakati anayefuata ni Majimaji mwenye pointi 24 na Njombe Mji yenye 22 itakuwa imeshuka rasmi.

Imefunga mabao yake matatu kupitia kwa Jacob Masawe dakika ya 3, Mrisho Ngassa ya 5 na Tibar John ya 40.

Hivyo kutokana na matokeo hayo, Ndanda inahitaji pointi moja tu itakayowafikisha pointi 27ambazo zinaweza kufikiwa na Majimaji pekee yenye 24 na hapo wataangalia tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa au ushindi wowote.

Mmoja kati ya hizo mbili itaungana na Njombe kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao, pia timu sita kutoka Ligi Daraja la Kwanza zitapanda ligi kuu kwa ajili ya msimu ujao utakaojumuisha klabu 20.