OUT wahofia mfumo mpya wa TCU

Muktasari:

Awali, wanafunzi waliomba kujiunga na chuo hicho moja kwa moja chuoni hapo.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa kuanzia mwaka huu, wanafunzi wanaotaka kujiunga (OUT) wanatakiwa kuomba kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). 

Awali, wanafunzi waliomba kujiunga na chuo hicho moja kwa moja chuoni hapo.

Naibu Makamu wa OUT, Profesa Deus Ngaruko amesema mfumo wa kutuma maombi TCU utawanyima watu wengi fursa ya kusoma na hivyo kurudisha nyuma lengo la uanzishwaji wa chuo hicho.

“Uelewa ni mdogo kuhusu majukumu ya chuo hiki kwa sababu wengi wa watoa uamuzi walisoma vyuo vya kawaida, lakini hapa tunapokea wanafunzi ambao hawakupata nafasi TCU, wafanyakazi na watu wazima wenye uhitaji wa kupata elimu kama Mwalimu Nyerere alivyotaka,” amesema.