Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FYATU MFYATUZI: Fyatu kuleta haki kwanza amani baadae



Juzi, nilipiga kanywaji hadi nikazimika na kuzimia kabla ya kuzimuliwa na Fyatuwe aka Bi Mkubwa. Si pale niliposikia mafyatu wakijifyatua, kujidanganya, na kudanganya wengine eti tuombe amani kwa kaya yetu bila kuwajua na kuwakomesha wavunja amani!

Ili iweje? Je, hapa, nani anajidanganya na kutaka kumfyatua nani? Hivi, kweli inawezekana kuwapo amani bila haki? Hawa wanaodai amani, kuivunja, kuiua, na kuipuuzia, wana akili kweli? Hivi, hawajui kuwa amani ni mtoto wa haki? Wapi kuliwahi kuwapo amani bila haki? Haki ni haki. Daima huvunja milima. Haki haitegemei amani kama ambavyo amani hutegemea haki.

Haki ya kweli haiwezi kuwapo bila amani. Haki siyo siasa wala sanaa bali haki. Yeyote anayetaa kuwapo amani bila haki anahitaji msaada tena wa bure. Huwezi kutetea haki kwa kudharau, kusahau, au kukandamiza haki.

Kama haki ni kiumbe, basi amani ni kizalia chake japo wote ni viumbe. Kama amani ni muhimu, haki ni lazima na muhimu. Yeyote anayekufyatua akidai uombee au kutetea amani bila haki anakugeuza bunga kama siyo zwazwa. Mkatae. Mkemee.

Na ikibidi mfyatue. Kwani, analenga kukufyatua. Hivi, kweli inawezekana jiwe kutoa maziwa achilia mbali maji? Sasa, inawezekanaje kuwa na amani bila haki? Haki ahitaji amani bali ukweli na uwajibikaji.

Amani inahitaji haki kwanza, na mengine yanafuatia hata yasipofuatia. Haki inaweza kushamiri bila kuhitaji msaada wa haki ila amani, bila haki, inakufa hata bila kupigwa kisu wala risasi.

Nasikia wengine, hasa mabambataa na mazwazwa wakiwahadaa mafyatu eti waombe amani! Wanakwenda mbali na kusema eti Fyatuland iombewe. Hapana. Fyatuland inahitaji kuambiwa tena ukweli kuwa mambo si mambo. Mtaomba hata utupu lakini amani haitakuwapo bila kuwapo haki. Fyatuland inahitaji kuambiwa kuwa bila haki hakuna amani. Na amani tunayoongelea hapa si ya wachache bali wote. Nani anataka amani ya wachache kula kwa amani wakati wengi wakinyimwa haki? Huu ni utani mbaya. Hayo, tuyaache kwanza.

Juzi, nilipita kwenye hekalu la tapeli mmoja aliitalo la Mungu. Msimuingize Mungu kwenye utapeli na usanii wenu. Mafyatu mazwazwa wengi walikuwa wakipiga mikelele wakiomba amani utadhani Sir God ni kiziwi!

Walipayuka kama machizi wakijihadaa wangemfyatua Sir God achanganywe na makelele ambayo matapeli wa kiroho waliojaa uroho hutumia kuwahadaa na kuwafyatua.

Wako wapi akina Gwjimy na matapeli wengine tena mazwaza? Hawa, waweza kuomba na kuleta amani kweli wakati maombi yao hayana amani achilia mbali imani?

Kama amani ni dunia, haki ni maji ambayo ndiyo chanzo cha kila kitu. Kama amani ni jengo au nyumba, basi haki ni msingi na sementi viianzishayo na kuihimili maisha yake yote. Kama ni gari, basi haki ni injini iendeshayo hili gari. Kama amani ni dhahabu, basi haki ni rhodium, osmium, na painite ambayo ni aghali kuliko yote duniani. Ngoja niache kuleta madude yetu maprofesa ili nisiwachanganye mafyatu na wasomaji wangu. Hayo tuyaache.

Tuanze kufyatuka na kutafakari pamoja. Hebu tujiulize na kujibu maswali haya pamoja tena kwa ukweli na uwazi. Kwanza, amani ni nini? Iko wapi na inapatikanaje na kwanini? Nini uzuri wa amani? Nani analinda, kujenga,au kuivunja amani? Bila kudurusu na kujibu maswali haya adhimu, tunajidanganya na kutaka kuwadanganya na kuwafyatua mafyatu waliogoma kufyatuka wakafyatua wawafyatuao.

 Pili, tujiulize. Tunajua tunachotaka au kutaka tusichojua?Je, tutakipataje na lini na kwa njia gani? Tunapaswa kuwa wakweli katika kuiendea na kuipata amani. Amani haitaki ubabaishaji, urongo na usanii. Japo tunaiita tunu, ni tunu gani ambayo hatuilindi na kuitunza kwa kufuata ukweli na usayansi wake?

Tatu, ni amani gani inaweza kuwapo na kushamiri katikati ya ubabaishaji, ukatili na uovu? Tunawezaje kuwa na amani ilhali wapo wenye haki ya kuwa nao hata kuivunja kuliko wengine?

Nne, ni amani ya nani na kwanini? Je, tumeweka misingi ya amani au ya imani ya amani kwa kuitelekeza hata kuichukia kama siyo kuiepa haki? Je, sheria na taratibu zetu zinajenga au kubomoa amani? Je, wanaowaibia wenzao na wanaoibiwa wanaweza kuwa na amani sawa?

Tano, kwanini hakuna amani? Na je, tumewahi kuwa nayo? Kama ilikuwapo, imekuwaje ikatoweka? Nini kimesababisha itoweke na tangia lini? Je, kama tulikuwa nayo, ilikuwa amani ya kweli au amani ya imani ya amani? Sita, je, nini kifanyike kuirejesha hii amani inayotuhangaisha?

Bila kujibu maswali haya na mengine, tunapoteza muda na kupigiana makeleke kwa kisingizio cha kusaka amani. Tutafute na kutenda haki kwanza.

Tukifanya hivi, amani itakuwapo na kutamalaki. Pia, tuhakikishe amani husika inakuwa ya wote na si ya baadhi. Kumbe kumekucha! Amani, we acha tu. Haki ziii! Amani hoyee!