Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi walijeruhi watu mkutano kujadili ukomo wa rais

Muktasari:

  • Mara baada ya Meya wa Jiji la Kampala Erias Lukwago kupanda jukwaani rabsha zilizuka baada ya polisi kufunga barabara karibu na eneo la mkutano mkabala na Makaburi ya Kasubi.

Watu wawili walikimbizwa jana hospitalini baada ya kuvuta hewa yenye moshi wa mabomu ya kutoa machozi na kupigwa na risasi polisi walipotawanya mkutano wa kuomba ushauri eneo la Kasubi tarafa ya Rubaga jijini Kampala.

Mkusanyiko huo uliandaliwa na Mbunge wa Lubaga Kaskazini, Moses Kasibante ili kuwahamasisha wananchi kuhusu haja ya kurekebisha Ibara ya 102 (b) ya Katiba inayozuia watu wenye umri zaidi ya miaka 75 kuwania urais

Baada ya mzungumzaji kusema hatua ya Mbunge wa Igara Magharibi Raphael Magyezi aliyewasilisha muswada ili kufuta ibara hiyo na kuungwa mkono na baadhi ya wabunge wa NRM inalenga kusafisha njia kwa Rais Yoweri Museveni kuwa “rais wa maisha” hivyo ni lazima kupinga.

Mkusanyiko huo umepewa jina la “Togikwatako”, ikiwa na maana Katiba isiguswe kaulimbiu inayotumiwa na Waganda wanaopinga marekebisho ya Katiba kwa lengo la kuondoa ukomo wa umri wa rais.

Mara baada ya Meya wa Jiji la Kampala Erias Lukwago kupanda jukwaani rabsha zilizuka baada ya polisi kufunga barabara karibu na eneo la mkutano mkabala na Makaburi ya Kasubi.

Katikati ya vurumai hizo polisi walipiga mabomu ya kutoa machozi. Mtu mmoja alijeruhiwa usoni na mwingine kwenye mguu wa kulia.

Wabunge wengi, madiwani na wanasiasa wengine walitoweka wakati maofisa wa polisi walirusha risasi mfululizo na mabomu ya machozi.

Kiongozi wa upinzani bungeni, Winfred Kiiza walipata makali ya moshi wa mabomu hayo.

Wasaidizi wake walimkinga ili kuhimili hewa ya mabomu iliyokuwa imetanda eneo lote la mkutano.

Naibu Meya wa Kampala Sarak Kanyike alizimia na alikimbizwa hospitalini.