Rais Magufuli aongoza mamia kumuaga Dk Masaburi

Muktasari:

Kauli ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa waombolezaji.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuuga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi aliyefariki Jumatano iliyopita na kusema Masaburi ana wake wanne au watano na watoto zaidi ya 20.

Kauli ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa waombolezaji.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza Dk Magufuli alisema anamfahamu Dk Masaburi kuwa alikuwa  na wake wanne au watano hivi.

Alisema hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20.

Rais Magufuli alisema Masaburi alikuwa rafiki yake,ndugu yake na mpiganaji mwenzake ndani ya CCM.