Rais Magufuli atengua uteuzi wa DCI

Rais Magufuli atengua uteuzi wa DCI Diwani

Muktasari:

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais Magufuli ametengua uteuzi huo leo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Diwani Athuman.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais Magufuli ametengua uteuzi huo leo.

Bila kutoa ufafanuzi wa sababu za mkuu huyo wa nchi kuchukua hatua hiyo, taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Athuman atapangiwa kazi nyingine.

“Kufuatia uamuzi huo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utatangazwa baadaye,” imeeleza sehemu ya taarifa kutoka Ikulu.