Ronaldo ageuka rapa akitambulishwa

Muktasari:

Ronaldo amepangwa kuanza katika mchezo wa leo utakaopigwa ugenini dhidi ya Chievo

Turin, Italia. Mshambuliaji mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo, ameyaanza maisha ndani ya klabu hiyo kwa kujiweka karibu na wenzake kwa kuwavunja mbnavu.

Licha ya ugeni alionao ndani ya Juve, mshambuliaji huyo mahiri na nahodha wa Ureno, aliwavunja mbavu wenzake na kuwakuna vilivyo wakati wa utambulisho wake mbele ya benchi la ufundi, wachezaji wenzake na viongozi wa juu wa Juventus.

Tofauti na wenzake ambao pindi waliposimama waliona haya, Ronaldo alimwambia DJ aongeze sauti na akaanza kuzirudi na kukutaka ukumbi mzima ukimpigia makofi ndipo alipoaanza kuyarudi magoma.

Ilibidi Ronaldo abakie kwenye kikoti cha utambulusho kwa muda mrefu kutokana naunenguaji wake kuwakuna wenzake wote ukumbini na kuwafanya wahudumu wasahau wajibu wao kwa muda na kumtizama mshambuliaji huyo alivyo mahiri katika unenguaji.

Ronaldo amepangwa kuanza katika mchezo wa leo utakaopigwa ugenini dhidi ya Chievo, akitarajiwa kufungua rasmi akaunti yake ya mabao.

Mshambuliaji huyo amepangwa kuongoza mashambulizi sambamba na wachezaji wenzake wapya, Joao Cancelo, Mattia Perin na Emre Can.

Ronaldo mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa Fifa wa ‘Fifa Ballon d’ Or’ anatarajiwa kurejesha mvuto wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ ambayo imefifia kwa sasa.

Serie ilitamba katika miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa 90 lakini ilipotezwa na ile ya Ufaransa na England katika miaka ya mwisho ya 1990 na ya 2000.