SSRA yazindua mfumo wa Tehama kwa wanachama

Ofisa wa SSRA David Nghambi

Muktasari:

Akizungumzia mfumo huo Ofisa wa SSRA David Nghambi alisema mfumo huo mpya utaiwezesha SSRA kupokea na kushughulikia malalamiko hayo moja kwa moja kwa wakati.

Dar es Salaam. Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii  nchini (SSRA) imeanzisha mfumo mpya wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  utakao wawezesha wanachama  kutuma na kufuatilia malalamiko yao.

Akizungumzia mfumo huo Ofisa wa SSRA David Nghambi alisema mfumo huo mpya utaiwezesha SSRA kupokea na kushughulikia malalamiko hayo moja kwa moja kwa wakati.

Alisema mfumo huo unaotambuliwa kwa jina la SSRA upo kwa njia ya mifumo ya simu (mobile application)na  unapatikana kwa njia ya simu za mkononi kupitia mtandao wa google hivyo mtu yeyote anaweza kuupakua na kuweka malalamiko yake.

"Mfumo huu hauna hatua nyingi kwani unakuingiza moja kwa moja katika ukurasa utakaokuwezesha kuingiza malalamiko yako na mamlaka itaweza kuyashughulikia" alisema