Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yalifungia Gazeti la Mwanahalisi miaka miwili

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi

Muktasari:

 

  • Serikali imesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari.

Dar es Salaam. Serikali imelifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili.

Imesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi ametangaza uamuzi huo leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari.

Dk Abassi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017.

Amesema kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

Amezitaja baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari "Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM".

Dk Abassi amesema, "Habari hii ilisheheni nia ovu dhidi ya Rais wakati suala husika lilihusu Shirika la Elimu Kibaha, wahariri walikiri udhaifu wakaomba radhi na kupewa onyo kali."

Amesema Gazeti la Mwanahalisi toleo la  jana lilichapisha makala yenye matusi, dhihaka na maneno yasiyofaa dhidi ya Rais John Magufuli.

"Tulipowaita wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa habari lazima izingatie maadili," amesema.