Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump aongoza matokeo ya uchaguzi Marekani

Muktasari:

Mbali na kuongoza katika majimbo hayo, wakati asilimia 89 ya kura zilikuwa zimehesabiwa mgombea huyo alikuwa akiongoza katika Jimbo la Florida kwa kura 18,000 zaidi dhidi ya Hillary; jimbo ambalo ili mgombea ashinde urais wa Marekani ni lazima apate ushindi jimboni humo

Matokeo ya awali yameendelea kutolewa katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika jana, ambapo hadi asubuhi hii mgombea urais wa Republican, Donald Trump alikuwa akiongoza kwa majimbo 60 dhidi 48 ya Hillary Clinton wa Democratic.

Mbali na kuongoza katika majimbo hayo, wakati asilimia 89 ya kura zilikuwa zimehesabiwa mgombea huyo alikuwa akiongoza katika Jimbo la Florida kwa kura 18,000 zaidi dhidi ya Hillary; jimbo ambalo ili mgombea ashinde urais wa Marekani ni lazima apate ushindi jimboni humo.

 Kambi ya Trump pia ilikuwa ikidai kuwa angeshinda katika majimbo ya Alabama, Arkansas, Indiana, Kentucky, Mississippi, Missouri, Oklahoma, South Carolina, Tennessee and West Virginia.

Matokeo yaliyokuwa bado kuthibitishwa katika majimbo ya Delaware, Rhode Island, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey, Rhode Island, Vermont  na District of Columbia yalionyesha kumpa ushindi Hillary.

Ili mshindi apate ushindi atatakiwa kupata ushindi unaofahamika kama ‘electoral college’ wa 270 dhidi ya mpinzani wake.