Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu hapa kocha mpya Yanga, wasifu umeshiba

Kocha mpya wa yanga, Manqoba Mngqithi.

Dar es Saalam. Yanga imemtangaza Manqoba Mngqithi kuwa Kocha wake Mkuu mpya akichukua mikoba ya kudumu ya Pedro Goncalves.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55, mara ya mwisho aliinoa Golden Arrows inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).

Kabla ya kuitumikia Golden Arrows, Mngqithi aliinoa Mamelodi Sundowns akiwa Kocha Mkuu na pia msaidizi.

Amewahi pia kuwa Kocha Msaidizi wa timu za Amazulu na Chippa United.

Ni kocha ambaye amekuwa akipendelea kutumia mfumo wa 4-3-3.

Ameshinda zaidi ya mataji 10 ya soka mojawapo likiwa ni la Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Mngqithi aliyezaliwa mwaka 1955, ni kocha mwenye leseni ngazi ya CAF Diploma A inayomruhusu kufundisha timu katika mashindano ya Klabu Afrika.

Yanga iliachana na Pedro Goncalves mwezi uliopita kutokana na kiwango kisichoridhisha cha timu hiyo.

Hata hivyo, Goncalves kwa sasa amepata fursa ya kuinoa AS FAR Rabat ya Morocco.