Uchaguzi Congo waahirishwa kwa miaka miwili
Rais wa Congo Joseph Kabila.
Muktasari:
- Mwandishi wa BBC, Mbelechi Msoshi, ameripoti taarifa hiyo na kueleza kuwa Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema serikali na viongozi wengine walifikia uamuzi huo.
Tume huru ya Uchaguzi ya Congo, imetangaza kuwa uchaguzi mkuu sasa utafanyika Novemba mwaka wa 2018 na wala sio mwaka huu kama ilivyotarajiwa.
Mwandishi wa BBC, Mbelechi Msoshi, ameripoti taarifa hiyo na kueleza kuwa Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema serikali na viongozi wengine walifikia uamuzi huo.
Viongozi kadha wa upinzani walioshiriki katika mazungumzo ya amani ya kitaifa wameafikiana na uamuzi huo, lakini kuna wale wanaoupinga wakisema ni njama ya Rais Joseph kabila kusalia madarakani.
Chanzo BBC