Ujerumani yamtia doa Trump
Muktasari:
Jarida la Der Sipeger la Ujerumani limenukuu taarifa iliyoandikwa na wizara hiyo ikisema Marekani itategemea kushuka kwa pato lake la ndani yaani GDP, viwango vya ajira na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira ikiwa Trump atapewa nafasi ya kulitawala taifa hilo.
Berlin. Wizara ya Uchumi ya Ujerumani imesema uchumi wa Marekani utaporomoka endapo mgombea wa urais wa Chama cha Republican, Donald Trump atashinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba 8 mwaka huu.
Jarida la Der Sipeger la Ujerumani limenukuu taarifa iliyoandikwa na wizara hiyo ikisema Marekani itategemea kushuka kwa pato lake la ndani yaani GDP, viwango vya ajira na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira ikiwa Trump atapewa nafasi ya kulitawala taifa hilo.
“Ikiwa Trump atashinda urais nchini Marekani uchumi wa nchi hiyo utaporomoka kwa kasi,’’ ilisema sehemu ya taarifa hiyo
Trump mwenyewe amekwisha kuahidi kuwa atashusha makato ya kodi kwa kiwango kikubwa katika historia ya Marekani akichaguliwa kuwa rais.
Kauli hiyo ya wizara ya Ujerumani inaongeza nyingine kama hizo zilizotolewa katika mfululizo wa ukosoaji dhidi ya Trump katika kipindi cha wiki iliyopita huku magazeti ya kihafidhina yakikataa kumuidhinisha mgombea huyo na hata wanasiasa wa Ujerumani kumshambulia moja kwa moja.
Mgombea huyo anachuana na mgombea wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton katika kinyang’anyiro hicho.