Vigogo Acacia wapandishwa kizimbani

Muktasari:

Viongozi wawili wa kampuni kubwa ya uchimbaji madini nchini ya Acacia, leo Jumatano Oktoba 17, 2018 wamepandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

Dar es Salaam. Aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Acacia, Deo Mwanyika na Alex Lugendo ambaye ni mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji fedha, kughushi na kula njama.

Mwanyika, Lugendo wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano, Oktoba 17, 2018 na kusomewa mashtaka yao, mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina huku wenzao wengine wanne wakiwa bado hawajafikishwa mahakamani.

Washtakiwa hao wamesoma mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Shadrack Kimoro na Jacqline Nyantole.

Katika shtaka la kwanza, ambalo ni la kula njama, linalowakabili Mwanyika na Lugendo,  wanadaiwa katika tarehe tofauti kati Novemba 11, 2008 na Juni 30, 2008 maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Kahama, Tarime, Biharamulo na katika maeneo ya Johannesburg, Afrika Kusini, Canada na Uingereza, washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

Mawakili wanaendelea kuwasomea mashtaka...

Endelea kufuatilia Mwananchi