Vigogo wa Chadema watinga mahakamani

Muktasari:

Jana Esther Bulaya aliunganishwa pamoja na wanachama wengine wanane katika kesi hiyo.

 


Dar es Salaam.  Wabunge wa Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wameshawasili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi saa 2.

Wabunge hao wanafika mahakamani kama walivyoamriwa na mahakama kutokana na mashtaka yanayowakabili, ikiwano ya kuhamasisha maandamano na uchochezi.

Miongoni mwa waliofika mahakamani ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Esther Bulaya wa Bunda, Halima Mdee (Kawe), Esther Matiko(Tarime Mjini), Naibu Katibu Mkuu bara, John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu .

Wamefika mahakamai hapo kutokana na kesi inayowakabili namba 112 ya mwaka huu 

Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ataongoza kesi hiyo huku  Wakili  wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi akijibu hoja zilizowasilishwa jana na Wakili wa utetezi Peter Kibatala.