Viongozi wawili CUF wajiuzulu

Muktasari:

Mzirai pia alikuwa mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho na Swedi alikuwa diwani wa Kata ya Kiwalani kupitia CUF.

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa CUF, Hashimu Mzirai na Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam, Musa Swedi wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama hicho leo.

Mzirai pia alikuwa mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho na Swedi alikuwa diwani wa Kata ya Kiwalani kupitia CUF.

Baada ya kutangaza uamzi huo wameomba kujiunga na CCM.

Msemaji wa CUF Abdul Kambaya amethibitisha kujiuzulu kwa viongozi hao huku akisema kuwa anayetakiwa kuulizwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Sief Shariff.

“Aulizwe Shariff ambaye ndiye huwa mnaona mwenye chama,”amesema.

 Hata hivyo aliendelea na kusema:

“Naibu Meya na Mwanasheria ambaye ndiyo alikuwa anamsimamia katika kesi zake zote naye ameondoka.”