Wachambuzi wa uchumi watoa neno kwa ATCL

Muktasari:

Wameeleza hayo ikiwa ni siku mbili baada ya Rais John Magufuli kupokea ndege mbili aina Bombadier Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka Canada kwa ajili ya kukuza uchumi, utalii na kulifufua shirika hilo

Dar es Salaam. Wachambuzi wa masuala ya uchumi wameeleza mambo yatakayoliendesha kwa mafanikio Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Wameeleza hayo ikiwa ni siku mbili baada ya Rais John Magufuli kupokea ndege mbili aina Bombadier Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka Canada kwa ajili ya kukuza uchumi, utalii na kulifufua shirika hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wamesema licha ya kuwapo kwa ushindani wa biashara, kuyumba kwa soko la usafiri wa anga, bado abiria wanaohitaji huduma hiyo wapo.

Wamesema mawakala wasiondolewe kwa kuwa hilo litaongeza gharama za uendeshaji na kulirudisha nyuma shirika hilo.