Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafuasi wa CUF watwangana tena mahakamani

Muktasari:

Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha pande mbili za chama hicho.

Dar es Salaam. Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa mara nyingine wametwangana tena makonde mahakamani.

Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha pande mbili za chama hicho.

Pande hizo ni  kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Ugomvi huo ambao umewahusisha walinzi wa viongozi wa chama hicho maarufu kama mabaunsa wa pande hizo mbili umezimwa na askari polisi sasa hivi.

Kwa sasa wafuasi wa pande zote wameingia mahakamani wanasubiri jaji aingie kwa ajili ya kusoma ya kusoma uamuzi wa maombi ya upande wa Maalim Seif kumtaka Jaji Sekieti Kihiyo anayesikiliza kesi hiyo ajiondoe kwa madai kuwa hawana imani naye.