Wakazi waliopisha Uwanja wa ndege Dodoma kulipwa kesho

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye

Muktasari:

Wakazi wa Dodoma walipisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma na walikuwa hawajalipwa fidia.

Dodoma. Wakazi wa Dodoma waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, wataanza kulipwa kesho.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amesema kila kitu kimekamilika hivyo hakuna sababu ya kulalamika.

Nditiye ametoa kauli hiyo bungeni leo septemba 11, 2018 wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Ferista Bura (CCM).

Mbunge huyo ametaka kujua ni lini wananchi wa Dodoma ambao nyumba zao zilivunjwa na kuwekewa alama ya X kwa ajili ya kupisha ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege.