Wananchi wafurika upimaji afya bure Mnazi Mmoja

Muktasari:

  • Muugizi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ziada Sellah amesema watu waliojitokeza ni wengi kuliko matarajio yao hivyo wamesitisha kupokea watu wapya ili kuhudumia waliokwisha sajiliwa.

Dar es Salaam. Idadi ya watu waliojitokeza kupima afya zao katika kampeni ya afya bure  imezidi kuongezeka hali iliyopelekea kusitishwa kwa utoaji wa namba za kuwasajili watu wapya ili kuhitimisha na waliokwisha sajiliwa hapo jana.

Muugizi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ziada Sellah amesema watu waliojitokeza ni wengi kuliko matarajio yao hivyo wamesitisha kupokea watu wapya ili kuhudumia waliokwisha sajiliwa.

"Idadi ya watu ni kubwa sana kuliko wahudumu ambao tunao kwa sasa hali ambayo hatukutegemea awali,"alisema Sellah.

Awali kampeni hiyo ililenga kutoa huduma kwa watu 3,000 lakini hadi kufikia jana ni zaidi ya watu 11,000 waliojitokeza, hadi kufikia leo saa 6 mchana ni watu 5,000 waliokwisha kupimwa afya zao.