Aishi Manula aongoza kikosi cha makipa Boko Veterans

Tuesday March 19 2019

 

KOCHA wa makipa wa Taifa Stars, Ahmad Emeka ameonekana kuwafua makipa wa  timu hiyo kuwa shapu ili wakabiliane ipasavyo na kashi kashi za washambuliaji wa Uganda.

Taifa Stars imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki AFCON miezi michache ijayo  nchini Misri.

Katika mazoezi yaliyofanyika asubuhi ya leo Jumanne kwenye Uwanja wa Boko Veterans, Emeka alikuwa akiwaweka mkazo kwa makipa ambao walikuwa wakishindwa  kufuata maelekezo yake.

Kocha huyo,  alipanga vituo kadhaa kupitia koni za mazoezi na kuanza kuwataka makipa wake mmoja baada ya mwingine kwa staili tofauti.

 Makipa ambao walikuwa wakinolewa na Emeka ni wanne kati yao waliwepo,  Aishi Manula,   Aaron Kalambo na Metacha Mnata.

Advertisement