Beki wa zamani Chelsea na Arsenal atangaza kustaafu soka

Muktasari:

Beki kisiki wa Timu za Arsenal na Chelsea raia wa Uingereza, Ashley Cole atangaza rasmi kutundika daluga katika mpira wa miguu.

Aliyekuwa beki wa zamani wa Chelsea na Arsenal, Ashley Cole amengaza rasmi kustaafu soka baada ya kutumika kwenye soka katika timu tofauti tofauti.

Cole alijiunga rasmi na Arsenal mnamo mwaka 1999 baada ya hapo akazitumikia Crystal Palace, Chelsea, Roma, LA Galaxy na Derby.

“Baada ya kukaa na kufikiria kwa muda mrefu nimeona ndio muda sahihi wa mimi kutundika daluga niangalie katika ukurasa unaofuata,” alisema Cole katika mahojiano yake na Sky Sports.

Pia amesema ni muda sahihi sasa wa yeye kutafuta sifa za kuchukua hatam za ukocha.

Beki huyo raia wa Uingereza amebeba jumla ya mataji 107 katika ligi ya England akiwa na vilabu tofauti tofauti pia ameshinda kombe la England mara mbili akiwa na Arsenal 2003-04.

Cole alijiunga na Chelsea mwaka 2006 akitokea katika timu ya Arsenal.

Vilevile ameshinda kombe la klabu bingwa barani ulaya (Uefa) akiwa katika klabu ya Chelsea mwaka 2011-12 na kombe la la Europa.

Baadaye alijiunga na Derby Country 2018 na kuwa chini ya kocha Frank Lampard aliyekuwa mchezaji mwenzie katika klabu ya Chelsea na kuiwezesha Derby kucheza fainali ya kupanda daraja dhidi ya Aston Villa.