China Open yambeba Kyle Edmund

Tuesday October 9 2018

 

Nyon, Uswisi. Mcheza tenisi mahiri wa Uingereza, Kyle Edmund, amepanda hadi nafasi ya 14 kwa ubora duniani akibebwa na matokeo ya michuano ya China Open, ambayo alifika nusu fainali.

Katika viwango vipya vya ubora viliyotolewa leo asubuhi na Shirikisho la Tenisi la Kimataifa (ITF) Edmund amepanda kwa kwa kiwango ambacho hajawahi kukifikia tangu ameanza kucheza tenisi.

Nyota huyo namba moja kwa ubora wa tenisi nchini Uingereza ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya 50 bora mwanzoni mwa mwaka huu anaweza kupanda zaidi iwapo atafanye vema katika mechi za mwisho mwa mwaka zitakazochezwa Desemba.

Edmund amemshusha aliyekuwa nyota wa nchi hiyo na namba moja wa zamani wa Dunia, Andy Murray, ambaye majeruhi yaliyomuweka nje kwa mwaka mmoja na nusu yamemfanya apotee kwenye ramani ya mchezio huo.

Mchezaji huyu mwenye miaka 23, alishinda mechi 13 mfululizo kabla ya kufungwa na Nikoloz Basilashvili katika nusu fainali ya China Open.

Advertisement