Hii ya Wawa, Murshid haijawahi kutokea!

Saturday January 12 2019

 

By Eliya Solomon

UKUTU wa mabeki wa kati,  Pascal Wawa na Juuko Murshid umeonekana kuwa na maelewano mazuri kwenye kikosi cha Simba SC baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura.

Ushindi wa mapema wa Simba SC dhidi ya JS Saoura  Ndani ya dakika 45 kipindi cha kwanza wa bao 1-0 iliisaidia timu hiyoya Mtaa wa Msimbazi kuja na mipango mizuri jambo lililowawezesha kuongeza mabao kipindi cha pili

Mara kadhaa imezoeleka kuonekana kwenye idara ya ulinzi ya Simba wakicheza Wawa na Erasto Nyoni kabla ya  kupata  majeraha kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar.

Mganda Juuko anaonekana kufiti kwenye nafasi ya Nyoni kwa kucheza kwa maelewano mazuri na Wawa ambaye ni kama kiungozi kwenye safu ya ulinzi ya Simba.

Mabeki hao walikuwa wakifanya kazi ya ziada kwa kuwasaidia walinzi wa pembeni wa Simba pindi ambapo walikuwa wakishindwa kuwadhibiti washambuliaji wa JS Saoura.

Katika mchezo huo wa  Ligi ya Mabingwa Afrika waliokuwa wakisaidiana na Wawa pamoja na Juuko kwenye safu ya ulinzi ya Simba SC ni Nicholus Gyan na Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Advertisement