VIDEO: Kaka azuia ndoa ya Samatta isitangazwe

Friday October 11 2019

 

By OLIPA ASSA

BABA  mzazi wa Mbwana Samatta,amefafanua hali halisi iliofanya ashindwe kujumuika na majirani zake kwenye ndoa ya mwanaye iliofungwa jana Alhamisi usiku, Mtongani eneo la Kichangani, Dar es Salaam.
Samatta anayekipiga Genk ya Ubeligiji, amemuoa mchumba wake wa muda mrefu Naima Mgange ambaye amezaa naye watoto wawili.
Ndoa hiyo ilikuwa ya kimyakimya, baada ya Mwanaspoti kufichua hilo, majirani wamemlalamikia mzee Ally Pazi Samatta kwamba hajawatendea haki.
Mzee huyo amejitetea kuwa wakati kaka yake Mbwana, Mohamed Samatta anayecheza KMC anafunga ndoa, kulikuwa na vurugu kubwa ambazo zilifanya maharusi wasahaurike.
"Samatta alihudhuria ndoa ya kaka yake, majirani wote walikuwa wanamshangilia Mbwana na sio Mohamed, sasa nikafikiria hili litakuaje,"
"Sikua na nia mbaya, Mbwana ni mtoto wao ndio maana huwa anakuja kuwatembelea na kuwasalimia, nilitaka wajue nilihofia fujo,"
"Mfano Wanahabari wangetangaza unadhani ingekuaje hapa, pamoja na kimyakimya umeona jinsi nyomi ya watu ilivyokuwa imejaa kwa mwanamke,"anasema.

Advertisement