Kamusoko huyooo! Hatimaye amerudi Yanga mwanangu

Wednesday February 14 2018

 

By Oliver Albert

 Yanga inaikabili Majimaji leo Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku mashabiki wa klabu hiyo wakifurahia kurejea kwa kiungo Thaban Kamusoko.

Kamusoko alikuwa majeruhi wa goti kwa muda mrefu tangu alipoumia Septemba mwaka jana katika mchezo dhidi ya Njombe Mji ambao Yanga ilishinda bao 1-0 ugenini.

Msemaji wa Yanga, Dismas Tena alisema Kamusoko amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na alifanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa leo.

"Kamusoko ni miongoni mwa majeruhi ambao wamepona na tayari wamerejea uwanjani na kufanya mazoezi na wenzake. Uamuzi wa kucheza dhidi ya Majimaji utabaki kwa makocha watakaoamua kama yuko fiti kutumika katika mchezo huo ama la," alisema Ten.

Yanga yenye pointi 34 inaikabili Majimaji huku ikihitaji ushindi kwa hali yoyote ili izidi kuwatia presha wapinzani wao wakubwa Simba walio kileleni na pointi 41.

Timu hiyo imeweka matumaini yote kwa mshambuliaji wao Obrey Chirwa mwenye mabao 10 ambaye hivi  sasa anamfukuzia kwa kasi Emmanuel Okwi mwenye mabao 13.  

Advertisement