Kiwango cha Luis Miquissone Simba SC cha mwibua Haji Manara mafichoni

Wednesday February 19 2020

 

By DORIS MALIYAGA

Dar es Salaam.Ukitaka kupambana na Haji Manara mbona utaipata, jamaa ana madongo ya maudhi kama ambavyo anawakera wapinzani wao Yanga.

Manara Afisa Habari wa Simba, eti anawaambia TFF na Bodi ya Ligi waongeze bei ya viingilio katika mechi zao kwa sababu wana wachezaji wanatoa burudani safi na haiendani na wanavyolipia.

Afisa huyo amemtaja winga wao mpya, Luis Miquissone raia wa Msumbiji, thamani ya kiwango chake iko juu.

"Kwa huyu Luis hata Azam TV ingebidi waongeze bei ya vifurushi vyao. Unajua mechi ya jana na Kagera Sugar nilikuwa namwangalia Luis nikajiuliza, nilikuwa namwangalia Messi au,"alihoji Manara.

Kiongozi huyo mwenye maneno mengi, alikwenda mbali na kusema, shabiki wa soka au Simba anapoamua kubaki nyumbani wakati Luis anacheza ni kosa kubwa.

Luis anayemwagiwa sifa na Manara ni mshambuliaji wao mpya, aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo kutoka UD Songo ya Msumbiji.

Advertisement

Kiwango cha mshambuliaji huyo ni kutokana na uzoefu wake wa kucheza mashindano tofauti katika ligi ya Afrika Kusini.

Advertisement