VIDEO: Lipuli, Simba wauteka mji wa Iringa

Tuesday February 26 2019

 

By Berdina Majinge

Iringa. Mji wa Iringa umesimama kwa muda wakati mashabiki Lipuli FC na Simba wakiwa katika hekaheka za kununua jezi na wengine kuingia kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Mtanange huu umechagizwa na vikolombwezo lukuki huku wafanyabiashara nao wakitumia fursa hiyo kuweka mambo yao sawa kwa kuuza bidhaa na huduma hasa chakula na malazi kwa wageni wa mji wa Iringa waliokuja kutazama mchezo huo.

Biashara iliyobamba zaidi kwa karibu wiki nzima ya maandalizi ya mchezo huo ni biashara ya jezi ambapo jezi inayouza zaidi ni ile ya Simba.

Mmoja wa wauza jezi Hamza Myovera alisema jezi zinazobamba leo kwa kununuliwa ni za Simba kwa sababu wauzaji wa jezi za Lipuli hawajajitokeza pia jezi hizo zinauzwa bei ghali.

Mvovera amewaomba uongozi wa Lipuli kushusha bei ya jezi na wao wapate kuuza kwa mashabiki.

Advertisement