Messi awabwaga Ronaldo, Van Dijk atwaa Ballon d'Or ya sita

Muktasari:

Awamu nyingine  ambazo Messi ametwaa BallondOr  ni  2009, 2010, 2011, 2012 na  2015. Mwaka jana tuzo hiyo, alitwaa  kiungo, Luka  Modric wa Real Madrid.

Paris, Ufaransa. Lionel Messi ameshinda  kwa mara ya sita tuzo ya  Ballon d’Or Jumatatu usiku  huku akiwazidi kete Virgil van Dijk wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

Messi  ambaye amefunga mabao 54 upande wa timu yake ya taifa ya Argentina  kuanzia mwaka 2018 hadi 2019,  anamataji 10  ya  Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga aliyotwaa akiwa na FC Barcelona.

Akizungumzia kutwaa kwa Messi tuzo hiyo,  Van Dijk ambaye alikuwepo katika sherehe za tuzo hizo huku Ronaldo akikosekana, alisema kufanya vizuri kwa mpinzani wake kumemfanya kuwema Historia.

"Nina furaha kwa namna nilivyokuwa na mwaka bora. Messi  ni bora katika historia? Amekuwa juu na ni kwa sababu ya kuwa ni mchezaji bora," alisema beki huyo, aliyeshika nafasi ya pili, nyuma ya Messi.

Awamu nyingine  ambazo Messi ametwaa BallondOr  ni  2009, 2010, 2011, 2012 na  2015. Mwaka jana tuzo hiyo, alitwaa  kiungo, Luka  Modric wa Real Madrid.

Orodha ya 10 bora ambayo ilikuwa inawania tuzo hiyo ambao ni 10.Riyad Mahrez, 9. Bernardo Silva, 8. Robert Lewandowski, 7. Alisson Becker, 6. Kylian Mbappe, 5. Mohamed Salah, 4. Sadio Mane, 3. Cristiano Ronaldo, 2. Virgil van Dijk  na 1. Lionel Messi.

Aliyetwaa tuzo ya BallonDor kwa wanawake ni Megan Rapinoe wa Reign FC. Tuzo ya kipa bora, imeenda kwa Alisson wa Liverpol inayofahamika kama 'Yachine Trophy'.

Matthijs de Ligt ambaye msimu uliopita alutesa akiwa na Ajax  ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani chini ya miaka 21, inayofahamika kwa jina la kopa trophy.