Mke wa Kobe Bryant afungua kesi kifo cha mumewe

Tuesday February 25 2020

 

Mjane wa Kobe Bryant Vanessa jana Jumatatu aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya waendeshaji wa helikopta iliyosababisha kifo cha mumewe Kobe Bryant, mtoto wake na watu wengine nane.
Shtaka hilo lilifikishwa katika Mahakama Kuu ya Los Angeles katika siku iliyofanyika shughuli maalumu ya kuwakumbuka kifo cha Kobe na wote walifariki katika ajali hiyo.
Katika ajali hiyo mbali ya Kobe wengine waliofariki ni Gianna Bryant na mchezaji mwenzake Alyssa Altobelli na Payton Chester, wazazi wa Altobelli John na Keri, mama wa Payton Sarah na kocha Christina Mauser.
Bodi ya Usalama wa Usafiri wa kitaifa bado inachunguza sababu ya ajali hiyo, ingawa matokeo ya awali hayakuonyesha ishara ya hitilafu ya mitambo.
Shtaka la Jumatatu linakosoa kampuni hiyo kwa kuruhusu helikopta kuruka katika "ukungu mzito na mawingu ya chini" Jumapili asubuhi, hali ambayo ilisababisha" baadhi ya kampuni nyingine kusitisha safari za helikopta zao.

Advertisement