Mourinho kumrithi Pochettino Spurs

Wednesday October 9 2019

 

London, England. Jose Mourinho anahusishwa na mpango wa kujaza nafasi ya Mauricio Pochettino Tottenham Hotspurs.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea and Manchester United, hana timu tangu alipotimuliwa Old Trafford Desemba, mwaka jana.

Pia Mourinho anahusishwa na mpango wa kujiunga na Real Madrid kujaza nafasi ya Zinedine Zidane.

Kocha huyo mwenye miaka 56, anaitolea macho Spurs ambayo kocha wake Mauricio Pochettino amekuwa kikaangoni.

Kipigo cha mabao kumi ndani ya wiki moja, kinamuweka Pochettino katika wakati mgumu Spurs.

Mourinho aliyewahi kuinoa Real Madrid, anaweza kupata wakati mgumu kurejea Santiago Bernabeu kutokana na uhusiano wake na rais wa klabu hiyo Florentino Perez.

Advertisement

Kocha huyo Mreno amekuwa akichambua soka katika televisheni kuhusu Ligi Kuu England.

Mourinho aliwahi kupewa ofa ya kurejea katika klabu yake ya zamani wa Benfica na aliahidiwa donge nono na Guangzhou Evergrande ya Ligi Kuu China.

Advertisement