Nick Minaj atangaza kuacha muziki

Friday September 6 2019

 

Marekani. Unaweza kujiuliza sababu ni nini lakini ukweli ni kuwa mwanamuziki wa Marekani, Nick Minaj ametangaza kuacha muziki ili apate muda wa kuwa na familia yake.

Ametoa kauli hiyo jana ambayo si ya kwanza kwake.

Mwaka 2014 aliwahi kutoa kauli kama hiyo katika wakati akihojiwa na jarida la Complex kwa madai kuwa umri wa kuwa na familia umefika.

“Umri wa kuzaa unazidi kusonga (alikuwa na miaka 31 wakati huo) sasa ana miaka 36, madaktari wanashauri muda mzuri wa mwanamke kuzaa usizidi miaka 35, naacha muziki nianzishe familia yangu, ”aliliambia Jarida la compex.

Jana Septemba 5, 2019, Minaj amerejea kauli hiyo kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Nimeamua kustaafu niwe na familia yangu najua kwa sasa mtakua na furaha, kwa mashabiki zangu endeleeni kushirikiana na mimi mpaka kifo changu,” amesema Minaj.

Advertisement

Tangu mwishoni mwa mwaka jana Minaj amekuwa kwenye mgogoro na rapa mwenzake Cardi B, kiasi cha bifu lao kuwagusa na mashabiki wao mitandaoni.

Agosti 13, 2019 Minaj na mpenzi wake Kenneth Petty walipata leseni ya ndoa iliyowataka kufunga ndoa ndani ya siku 80.

Huenda jambo hilo ndio limeibua minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake wakiamini kuwa inawezekana rapa huyo ana ujauzito na anajipanga kuingia kwenye ndoa akiwa ametulia.

Mpaka sasa Minaj ameachia jumla ya albums 4, Singles 105, Mixtapes 3 na Compilation albums 3.

 

Advertisement