Nyoni, Juuko na Kwasi wapiga tizi peke yao

Thursday February 14 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mabeki Erasto Nyoni, Juuko Murshid na Asante Kwasi leo wamefanya mazoezi peke yao wakati Simba ikijiandaa na mechi dhidi ya Yanga keshokutwa Jumamosi.

Nyoni alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi tangu alipoumia katika kombe la Mapinduzi Zanzibar wakati Kwasi na Juuko waliumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe aliwapangia mazoezi ya kufanya huku Juuko na Nyoni walikuwa wamepangiwa mazoezi ya kuendesha baiskeli.

Beki Pascal Wawa alikuwa anafanya mazoezi ya viungo akiwa chini kabla ya kujiunga na wenzake Nyoni na Juuko.

Advertisement