Okwi ajifua kuwakabili AS Vita

Wednesday March 13 2019

 

Kikosi cha Simba kilicheza mechi ya ugenini katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ua JSS na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0. Kikosi hicho mbali ya kufungwa kulikosa huduma ya mshambuliaji wake Emmanuel Okwi ambaye aliachwa kutokana na kuwa mgonjwa.

 Wiki hii kulikuwa na taarifa za mitandaoni kuwa Okwi ameondoka na kwenda kwao Uganda.

 Katika mazoezi ya kujindaa na mechi ya AS Vita ambayo Simba watacheza Jumamosi uwanja wa Taifa Okwi alionekana akiwa anafanya mazoezi ya pamoja na wenzake.

 Kikosi hiko cha Simba kilifanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterans leo kuanzia saa 10:00 jioni.

Advertisement